JKIA
News

Mzozo kuhusu usimamizi wa JKIA

Mzozo kuhusu usimamizi wa JKIA washika Kasi.

Hatma ya  mkataba wa kuruhusu shirika la ndege la KQ  kusimamia operesheni zote katika uwanja wa kimtaifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) sasa haijulikani.

Hii ni baada ya pande zote husika yaani KQ na halmashauri ya usimamizi wa Nyanja za ndege kutofautiana kuhusu wao kusaini mkataba huo.

Read Also: How Pastor Alph Lukau raised a dead man

Akiwa mbele ya kamati ya bunge kuhusu uchukuzi,afisa mkuu mtendaji wa KAA Johny Anderson amekiri KQ imepokea mkataba huo ila haujaidhinisha kufuatia hofu zake kuhusu mpango wenyewe.

Naye   mkurugenzi mkuu wa KQ  Sebastian Mikosz akitetea pendekezo lao amesema KQ haikulenga kutwaa JKIA ila ilinuia kupandisha hadhi ya uwanja huo muhimu ili kupiku wapinzani wake aliyetaja kama vile Ethiopia,Etihad,Rwanda na Emirates.

Read Also: KRA freezes accounts of African Spirits Ltd tycoon

Kwa sasa kamati ya bunge la kitaifa kuhusu uwekezaji wa umma chini ya uongozi wa Abdulswamad Nassiri imependekeza mkataba huo kusitishwa kwa muda hadi mkaguzi wa serikali Edward Ouko kuufanyia kazi.

2 COMMENTS

LEAVE A RESPONSE

Your email address will not be published.