Oparanya
News

Gavana Oparanya asisitiza atawania urais mwaka wa 2022


Gavana wa kaunti ya Kakamega na ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la magavana nchini COG Wycliffe Oparanya ameapa kuwania kiti cha urais nchini mwaka wa 2022.


Akizungumza katika kituo kimoja cha televisheni nchini,  gavana Oparanya amesema kwamba yuko tayari kuwania kiti hicho na wawaniaji wengine ingawa hakukitaja chama ambacho atakitumia kuwania. 

Read Also:Expired rice impounded in Kariobangi


Ikumbukwe kwamba wengi wa viongozi wamekuwa na uchu wa kuwania kiti cha urais mwaka wa 2022 haswa baada ya kuwepo kwa mazungumzo kuhusiana na vita dhidi ya ufisadi.


Kwa sasa wakenya wana kibarua kikubwa kuona iwapo vita dhidi ya ufisadi,  ajira kwa vijana,  uongozi kando na uwanasiasa na vile vile kupunguzwa kwa gharama ya maisha zitaangaziwa kikamilifu.

LEAVE A RESPONSE

Your email address will not be published.